Jina kamili la msanii huyu ambaye maetengeneza filamu nyingi zilizotia fora katika matamasha mengi ya filamu za sinema ni Abid Mohammed Medoun Hondo aliyezaliwa mwaka 1936 nchini Mauritania. Alihamia Ufaransa mwaka l954 ambako bada ya juhudi kubwa, licha ya matyatizo ya kimaisha alitengeneza filamu yake ya kwanza E Soleil)i katika mwaka 1969. Atakapokuwepo Zanzibar, miongoni mwa filamu maarufu za msanii huyu zitakazoonyeshwa ni Sarraunia (1986) na Watanii (1998). Sarraunia ni filamu ya Malikia wa Mali ambaye aliongoza majeshi yake katika mapambano makali, ijapokuwa yalichukua muda mfupi na yaliyopoteza maisha ya watu wengi dhidi ya kikoloni ya Wafaransa . Filamu hii inayotokna na tukio la, kweli inaonyesha jinsi wanawake wa Kiafrika walivyoweza kuongoza nchi na kwa kutumia pia mazingaombwe walivyokataa utawala wa kigeni na kutaka kulinda heshima na mila yao. Filamu nyengine ni za Wasanii wa Iran, Japan, Denmark, Australia, Iran, Afrika ya Kusini, Ujerumani, Morocco, Ufaransa, Marekani, Cameroon, Tunisia, Msumbiji, Nigeria na Tanzania. Miongoni mwa filamu hizi ni ile ya Kwa nini uliwaua jirani zetu? . Hii ni filamu ya kusikitisha, lakini yenye lengo la kutoa fundisho kwa nchi za Kiafrika juu ya umuhimu wa kusahau yaliyopita, kuvumiliana na kusihi pamoja kama ndugu watu wa makabila na silka tafauti, iwe katika nchi moja au nchi jirani. Filamu hii iliyoongozwa na Mjapani, Kumiko Igarashi iliyotengenezwa mwaka 1997 inahusu mauaji ya halaiki nchini Rwanda ambapo Wahutu walio wengi waliwaua Watutsi ambao kwa maisha ya Kiafrika walitakiwa wawe watani wao wapatao laki nane. Katika filamu hii, kijana mmoja aliyetoka jela aaelezea jinsi alivyolazimishwa kuwaua watoto wa dada zake na jinsi vyombo vya habari vilivyotu-miwa vibaya kuchochea mauaji haya ya kiwenda wazimu. Pia ipo filamu iitwayo Kumbukumbu na Ndoto iliyotengenezwa mwaka 1999 iliyotengenzwa na Dk. Ibrahim Mokhtari, Mfaransa mwenye asili ya Iran. Inaelezea habari za mwanamke wa kijijini nchini Iran aliyekuwa akimiliki ng'ombe . Siku moja watoto wake walimuuza yule mnyama bila ya kumwambia. Siku moja akiwa amejaa huzuni na mfa-dhaiko alianza kuchora kuta, maboga na chochote alichokiona kilifaa kuchorwa ili kupunguza majonzi mpaka pale mmoja wa watoto wake alipozuru Teheran, mji Mkuu wa Iran ambako alimnunulia karatasi na rangi. Tokea hapo kizee hiki kikajihusisha na kuchora bila ya mapumziko ya muda mrefu ju ya maisha yake ya shida na dhizki zisio na kifani, na hasa juu ya ugomvi usiokwisha na wake wenza wenzake, wanawake wenzake kijijini. Picha hizi zni za kusikitisha, lakini zenye kutoa mafunzo memgi, hasa juu ya shida za akina mama vijijini na masururu wa mateso wanayopambana nayho, baadhi ya wakati kutoka kwa watoto waliowazaa wenyewe. Zipo filamu zinzoonyesha na kueleza historia ya Bagamoyo, Mji Mkongwe wa zanzibar na maisha ya Watanzania. Muandishi |