Jukwaa la Muziki
Wasanii husema muziki ndio chakula cha mapenzi, lakini pia wapo wanaosema muziki ndio kirutubisho mwanana wakati wa kula na hata kulala. Tamasha limeandaa muziki mchanganyiko kutoka kila pembe ya dunia... ile miondoko ya mwendo wa konokono, pole pole iliyojaa madaha, kasi kama ile ya jahazi pale upepo mkali unapovuma na vimbwaga vya nataka tikisa bodi langu. Uchaguzi ni wa mtazamaji na msikilizaji.

Miongoni mwa vikundi vitakavyoshiriki katika tamasha hili ni kile cha Tyoussi Medd, raia wa ufgaransa mwenye asili ya Morocco, Maalesh (Sio Kitu) kutoka Comoro na Salamat kutoka Misri ambaye ameamua kukatiza ziara yake ya nchi za Ulaya ili kuungana na nchi za majahazi katika tamasha hili la aina yake. Watakuwepo wana muziki kadha maarufu kutoka nchi mbali mbali za Ulaya, Ghana, Tanzania Bara na Visiwani.

 

Muandishi
Said Salem